Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 21:34

Rais wa Madagascar agombea kuchaguliwa tena katika uchaguzi utakaofanyika Alhamisi


Rais wa Madagascar aliyeko madarakani Andry Rajoelina akiwa katika kampeni huko Mahanoro Novemba 11, 2023 akiomba kuchaguliwa tena (Picha na RIJASOLO / AFP.
Rais wa Madagascar aliyeko madarakani Andry Rajoelina akiwa katika kampeni huko Mahanoro Novemba 11, 2023 akiomba kuchaguliwa tena (Picha na RIJASOLO / AFP.

Rais wa Madagascar anagombea kuchaguliwa tena Alhamisi huku nchi ikikabiliwa na wiki kadhaa za maandamano kutoka makundi ya upinzani ambayo yanasema kwamba hana sifa za kugombea na uchaguzi lazima ucheleweshwe.

Andry Rajoelina mwenye umri wa miaka 49 mjasiriamali na Dj wa zamani aliingia madarakani katika mapinduzi ya mwaka 2009 ambayo yaliwatia khofu wawekezaji katika taifa hilo la kisiwa lililoko kwenye bahari ya Hindi.

Alijiuzulu baada ya takriban miaka mitano kama kiongozi wa utawala wa mpito na baadae alikuwa rais baada ya kushinda uchaguzi wa mwaka 2018.

Maafisa wanasonga mbele na mipango ya uchaguzi wa duru ya kwanza Alhamisi siku chache baada ya kiongozi huyo wa baraza kuu la bunge, mwanachama wa chama cha rais mwenyewe kutaka upigaji kura huo isitishwe kwa sababu masharti hayakuwa sawa.

Zaidi ya wiki sita polisi wametumia gesi ya machozi kuvunja maandamano ya mara kwa mara ya wafuasi wa wapinzani wa kisiasa wa Rajoelina ambaye wanasema hana sifa kwa sababu alichukua uraia wa ufaransa mwaka 2014.

Forum

XS
SM
MD
LG