Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 20, 2025 Local time: 10:38

Rais wa Liberia sasa ni mwenyekiti wa ECOWAS


Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, amechukua uongozi wa jumuiya ya uchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS akiahidi kudumisha amani na usalama na kuwataka nchi wanachama kufanya kazi kwa bidii zaidi kupambana na ugaidi.

Rais Sirleaf anachukua nafasi hiyo kutoka kwa Rais Macky Sall wa Senegal. Uchaguzi ulifanyika katika mkutano wa ECOWAS uliofanyika mwishoni mwa juma katika mji mkuu wa Senegal Dakar.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Ofisi ya Rais imesema Rais Sirleaf alitoa wito wa kumaliza mazungumzo na hatua za kisheria ili kuinua utengamano wa kibiashara Afrika Magharibi.

Mwenyekiti huyo mpya wa ECOWAS ameahidi atafanya kazi kuinua uthabiti wa kiuchumi.

XS
SM
MD
LG