Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 08, 2024 Local time: 16:12

Rais wa Ivory coast ateua ndugu yake kuwa waziri wa ulinzi


Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara (katikati) akiwa pamoja na baadhi ya viongozi serikalini. April 19 2022. PICHA: AFP
Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara (katikati) akiwa pamoja na baadhi ya viongozi serikalini. April 19 2022. PICHA: AFP

Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara ameteua baraza la mawaziri 32, ikilinganishwa na 41 katika baraza lililoondoka siku chache zilizopita.

Mawaziri wa ulinzi, na mambo ya nje wamesalia katika nafasi zao, japo amemteua waziri mpya wa wizara ya madini.

Ouattara alikuwa ameahidi kupunguza idadi ya mawaziri baada ya waziri mkuu Patrick Achi kuasilisha maombi ya serikali yake kujiuzulu mnamo April 13.

Achi hata hivyo aliteuliwa katika nafasi hiyo siku chache baadaye.

Ouattara amemteua aliyekuwa gavana wa benki kuu ya nchi hiyo ya Afrika magharibi Tiemoko Meyliet Kone kuwa makam wa rais.

Idadi kubwa ya mawaziri waliokuwa katika baraza lililopita wamerejeshwa ofisini, akiwemo ndugu ya rais Ouattara Tene Birahima Ouattara ambaye ni waziri wa ulinzi.

Ouattara anatarajiwa kumaliza mhula wake madarakani mwishoni mwa mwaka 2025.

XS
SM
MD
LG