Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 05:03

Rais wa Ivory coast akutana na marais wa zamani kwa ajili ya umoja wa taifa


Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara (kulia) baada ya mkutano na waliokuwa marais Laurent Gbagbo (katikati) na Henri Konan Bedie (kushoto) katika ikulu ya rais mjini Abidjan. July 14 2022. PICHA: AFP
Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara (kulia) baada ya mkutano na waliokuwa marais Laurent Gbagbo (katikati) na Henri Konan Bedie (kushoto) katika ikulu ya rais mjini Abidjan. July 14 2022. PICHA: AFP

Rais wa Ivory coast Alassane Ouattara amekutana na marais wa zamani wa nchi hiyo kwa mazungumzo namna ya kuleta hali ya utulivu nchini humo.

Outttara amefanya mazungumzo na waliokuwa marais Henri Konan Bedie na Laurent Gbagbo katika ikulu ya rais.

Viongozi hao watatu wametawala siasa za Ivory coast kwa miongo mitatu.

"Mkutano wa leo ni wa kubadilishana mawazo kuhusu maswala muhimu yanayohusu nchi. Rais wa Jamhuri na watangulizi wake wameonyesha nia ya kuufanya mkutano huu kuwa mwanzo wa mchakato wa kuboresha hali ya kijamii na kisiasa nchini Ivory Coast.” Amesema Outtara

Akikaimu kama msemaji wa kikao hicho, Gbagbo amesema kwamba wanataka mkutano huo wa kwanza utakuwa mwanzo wa kuboresha maswala ya kitaifa, kijamii na kisiasa nchini humo.

Hali ya kisiasa imekuwa ikiyumba nchini Ivory Coast kwa mda.

Mnamo mwaka 2010, Gbagbo alikataa kuondoka madarakani licha ya kushindwa na Allasane Ouattara katika uchaguzi mkuu.

Karibu watu 3000 waliuawa katika vita vya mda mfupi vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo, kabla ya waasi waliokuwa wanamuunga mkono Ouattara kuingia mjini Abidjan kwa mapigano.

Gbagbo aliondolewa mashtaka ya uhalifu wa kibinadamu katika mahakama ya uhalifu ya kimataifa ICC mwaka 2019.

Amerudi Ivory Coast mwaka uliopita.

Ouattara amesema kwamba mkutano huo ni muhimu sana na utakuwa ukifanyika kila mara.

"Nadhani litakuwa jambo zuri kwa taifa kuwasikiliza viongozi wa zamani na kutumia busara yao na uzoefu wao wa kisiasa. Tutakuwa na fursa ya kukutana kila mara nafasi ikipatikana.

Ouattara ameleta hali ya utulivu nchini Ivory Coast wakati wa utawala wake, lakini Darzeni ya watu kadhaa waliuawa wakati wa uchaguzi wa mwaka 2020.

Ouattara alikuwa anagombea uraia kwa mhula wa tatu wakati wa uchaguzi huo, hatua ambayo Gbagbo na Bedie walisema ilikuwa kinyume cha sheria.

XS
SM
MD
LG