Hotuba hiyo imekuja katikati ya wasiwasi wa Marekani kuhusu juhudi za Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kuleta mageuzi katika mfumo wa mahakama na kupanua makazi ya Wayahudi katika maeneo ya Wapalestina yanayokaliwa kimabavu na Israeli.
Baraza la Wawakilishi la Marekani lilipitisha azimio Jumanne kuimarisha ungaji mkono wa Marekani kwa Israeli.
Azimio hilo limekuja ikiwa ni majibu kwa maoni ya mbunge Mdemokrat.
Pramila Jayapal, aliita Israeli ni “taifa la kibaguzi “ kabla kufafanua baadaye kuwa anaamini serikali ya Netanyahu “ imejihusisha na ubaguzi na sera za wazi za kibaguzi na kuwa kuna wale ambao wenye msimamo mkali wa kibaguzi wanaosukuma sera hizo ndani ya uongozi wa serikali iliyoko madarakani.
Wabunge kadhaa Wademokrat wamesema watasusia hotuba ya Herzog, akiwemo mwakilishi Rashida Tlaib, mmarekani mwenye asili ya kipalestina ambaye ni pekee katika Bunge.
Wabunge kadhaa wamesusia hotuba za viongozi waliotangulia, ikiwemo hotuba ya Waziri Mkuu wa India Narendra Modi i katika Bunge mwezi uliopita.
Baadhi ya taarifa katika ripoti hii zinatokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.
Forum