Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 02:52

Rais wa Ghana asema mazungumzo na IMF yanaendelea vizuri

Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo akitabasamu wakati wa mazungumzo na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwenye Ikulu ya Elysee mjini Paris, Ufaransa, Oktoba 13, 2022. (REUTERS)
Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo akitabasamu wakati wa mazungumzo na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwenye Ikulu ya Elysee mjini Paris, Ufaransa, Oktoba 13, 2022. (REUTERS)

Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo Jumapili alisema mazungumzo na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF yanaendelea vizuri na kutaka kuwahakikishia wawekezaji kwamba mazungumzo hayo hayatasababisha kupunguzwa kwa thamani ya dhamana za serikali.

Hotuba ya rais kwa taifa ilitaka kuwahakikishia Waghana na masoko kwamba serikali inaweza kukabiliana na mzozo wa kiuchumi ambao umeilazimisha kugeukia Mfuko huo kwa usaidizi wa kifedha.

Mazungumzo "yako katika hatua za juu, na yanaendelea vizuri," Akufo-Addo alisema.

Hakuna mwekezaji binafsi au taasisi itapoteza fedha zake kutokana na mazungumzo yetu na IMF yanayoendelea. Hakutakuwa na kupunguzwa thamani ya mali alisema, na kukashifu kama uvumi wa uwongo ripoti za hivi karibuni za uwezekano wa urekebishaji kama huo.

Ghana ilianzisha mazungumzo na IMF mwezi Julai wakati wawekezaji wa kigeni wakitupilia mbali madeni yake na maandamano ya mitaani yalizuka kutokana na msukosuko wa kiuchumi ambao umeshuhudia mfumuko wa bei na kushuka kwa thamani ya fedha kufikia viwango vya juu licha ya kuongezeka mara kwa mara kwa kiwango kikubwa cha viwango vya riba ya mikopo.

XS
SM
MD
LG