Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 14:54

Rais wa Ghana afanya ziara Marekani


Rais wa Ghana John Evans Atta Mills akisalimiana na rais Obama huko White House.
Rais wa Ghana John Evans Atta Mills akisalimiana na rais Obama huko White House.

Rais wa Ghana afanya ziara Marekani na Rais Obama aelezea maendeleo ya Ghana kama “ hadithi nzuri ya mafanikio ya kiuchumi barani Afrika”.

Rais wa Ghana John Atta Mills alikutana Alhamisi na Rais Barack Obama wa Marekani katika White House ambapo Bw.Obama alisifu maendeleo makubwa yaliyofikiwa na taifa hilo la Ghana. Bw.Obama aliwaambia waandishi wa habari baada ya mkutano kati yake na rais Mills kwamba rais huyo wa Ghana amebaini wazi ahadi yake ya kupambana na rushwa na uwajibikaji katika utendaji kazi nchini mwake kwa kuzingataia utawala wa kidemokrasia. Bwana Obama aliyaelezea maendeleo hayo kama “ hadithi nzuri ya mafanikio ya kiuchumi barani Afrika”.Viongozi hao wawili walisisitiza kuwa nchi zao zimetimiza hatua ya kidemokrasia . Rais Obama alisema Ghana imedhihirisha kuwa mfano mwema barani Afrika katika swala la kidemokrasia na kushukuru jitihada za rais Mills za kuhakikisha uchaguzi huru n wa haki. Alisema serikali ya Ghana inawajibikia raia wake na wala sio wachache tu.

Na akitoa shukrani zake kwa rais Obama kwa kuonyesha heshima kuu kwa kutembelea Ghana mwaka 2009, rais Mills alisema nchi hizi mbili zinathamini demokrasia. Rais Mills anatazamiwa kugombea kiti cha rais kwa muhula wa pili mwezi Desemba.

XS
SM
MD
LG