Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 22:57

Rais wa Eritrea Afwerki aepuka kujibu maswali wakati wa ziara yake Kenya


Rais wa Eritrea Isaias Afwerki akiongea katika mkutano wa waandishi wa habari alioufanya pamoja na Rais wa Kenya William (hayuko katika picha) mjini Nairobi, Kenya.
Rais wa Eritrea Isaias Afwerki akiongea katika mkutano wa waandishi wa habari alioufanya pamoja na Rais wa Kenya William (hayuko katika picha) mjini Nairobi, Kenya.

Rais wa Eritrea Isaias Afwerki Alhamisi aliepuka kujibu maswali kuhusu wanajeshi wa nchi yake kubaki katika mkoa wa Tigray nchini   Ethiopia  miezi mitatu  baada ya kusaini mkataba uliowataka  waondoke.

Wanajeshi wa Eritrea walipigana sambamba na jeshi la Ethiopia na wanamgambo washirika wakati wa mzozo wa miaka miwili dhidi ya majeshi ya Tigray.

Wanajeshi hao wa Eritrea wameshutumiwa na wakazi wa eneo hilo na vikundi vya haki kwa unyanyasaji uliokithiri, ikiwemo tuhuma za mauaji na ubakaji. Maafisa ya Eritrea wamekanusha tuhuma hizo.

Wakazi na wanadiplomasia wa kigeni wamesema wanajeshi wengi wa Eritrea bado wako Tigray licha ya kuwa wameondoka katika miji mikubwa kadhaa.

Kujitokeza kwa Rais Isaias ambapo ni nadra kukutana na vyombo vya habari vya kimataifa, lakini katika ziara yake mjini Nairobi, alishiriki mkutano wa pamoja wa vyombo vya habari na rais wa Kenya William Ruto.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG