Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 18:54

Rais wa Colombia Juan Santos hajaridhika na matokeo ya kura ya maoni


Rais wa Colombia, Juan Manuel Santos
Rais wa Colombia, Juan Manuel Santos

Viongozi wa kisiasa nchini Colombia wanaangalia njia ya kusonga mbele baada ya wapiga kura kukataa mkataba wa amani na waasi wa FARC wa mrengo wa kushoto mkataba ambao ungemaliza miaka 52 ya vita.

Rais Juan Manuel Santos alipanga kukutana Jumatatu na vyama vyote vya kisiasa na amewaagiza wapatanishi wake kurudi mjini Havana nchini Cuba mahala ambako mazungumzo ya amani yalikuwa yakifanyika kwa miaka minne.

Asilimia 50.2 ya wapigakura wa Colombia walikataa mkataba huo dhidi ya asilimia 49.7 ya waliounga mkono. Rais Santos na viongozi wa waasi wanaapa kushinikiza kusonga mbele na utaratibu wa kura japokuwa haijafahamika wazi ni namna gani wanavyoweza kuokoa mkataba huu kwa kuwa inaonekana hakuna mpango wa ziada.

XS
SM
MD
LG