Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 18, 2025 Local time: 14:03

Rais wa Chuo Kikuu cha Harvard ajiuzulu


Rais wa chuo kikuu cha Harvard, Claudine Gay, amesema atajiuzulu katika nafasi yake Jumanne, baada ya miezi yake ya mwanzo katika nafasi yake kukumbwa na kutoa ushuhuda katika bunge kuhusu shutuma za ubaguzi na wizi wa kazi za kitaaluma.

Gay alikabiliwa na shinikizo la kujiuzulu kutoka kwa jumuiya ya kiyahudi ya Havard, na baadhi ya wabunge kutokana na maoni yake katika mahojiano katika bunge ya Desemba 5, na toka kipindi hicho amekuwa akikabiliwa na shutuma kadhaa za wizi wa kazi za kitaaluma katika kazi zake za kitaaluma katika mieizi ya hivi karibuni.

Katika barua yake ya kujiuzulu kwa jamii ya chuo kikuu cha Havard, Gay amesema uamuzi wake wa kujiuzulu umekuwa ni mgumu kuliko namna anavyoweza kujieleza.

Forum

XS
SM
MD
LG