Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 10:00

Rais wa China Xi Jinping aonya majirani zake wa Asia ya kati

Rais wa China Xi Jinping.(AP/Pavel Golovkin)
Rais wa China Xi Jinping.(AP/Pavel Golovkin)

Rais wa China Xi Jinping ameonya majirani zake wa Asia ya kati katika hotuba yake ya  Ijumaa dhidi ya kuruhusu watu wa nje kuwadhoofisha na mapinduzi ya rangi shirika la habari la taifa la Russia limeripoti.

Shirika hilo limeripoti likigusia kuhusu maandamano yaliyopindua utawala wa zamani wa Kisoviet na mashariki ya kati.

Maelezo ya Xi katika Mkutano wa usalama na rais wa Russia Vladmir Putin na viongozi wa Asia ya kati, India , na Iran zinaonyesha wasiwasi wa China kwamba uungaji mkono wa magharibi kwa wanaharakati wa demokrasia na haki za binadamu ni njama ya kudhoofisha Chama Cha Kikomunisti cha Xi na serikali zingine za kimabavu kwa sasa, mageuzi ya mabadiliko makubwa ambayo hayajaonekana katika karne moja duniani yanashika kasi, dunia imeingia katika kipindi kipya cha misukosuko na mabadiliko. Tunapaswa kufahamu mwenendo wa nyakati , kuimarisha mshikamano na kuendeleza ujenzi wa jumuiya ya karibu ya mustakabali wa pamoja wa shirika la ushirikiano la Shangai" amesema Rais Xi Jinping.

Mkutano huo ni sehemu ya safari ya kwanza ya Xi nje ya nchi tangu kuzuka janga la Corona lililozuka miaka miwili na nusu iliyopita ikisisitiza umuhimu wa Beijing wa kukuza matarajio yake ya kimkakati.

XS
SM
MD
LG