Rais wa China Xi Jinping amerudia kusema tena ushirikiano wake usiokua na mipaka wakati wa mazungumzo ya simu na Rais wa Russia Vladimir Putin leo Jumatatu vyombo vya habari vya serikali ya China vimeripoti katika maadhimisho ya miaka mitatu ya uvamizi kamili wa Russia nchini Ukraine.
Viongozi hao walifanya mazungumzo hayo wakati Rais wa Marekani Donald Trump akishinikiza kufikiwa kwa makubaliano ya haraka kumaliza vita vya Ukraine na kuongeza matumaini kwamba Marekani inaweza kuwatenganisha Xi na Putin na hivyo kujikita katika kushindana na taifa la pili kubwa kiuchumi duniani.
Mazungumzo hayo ya simu yanaonekana yalikuwa na lengo la kuondoa matarajio yoyote kama hayo, ambapo viongozi hao wawili walisisitiza uimara na hali ya muda mrefu ya ushirikano wao wenye nguvu zake maalum ambayo haitaweza kuathiriwa na mtu mwengine.
Trump amewashangaza washirika wake wa Ulaya kwa kutowahusisha na suala la Ukraine kutokana na mazungumzo na Russia wiki ilyiopita ikilaumu Ukraine kwa kuanzisha uvamizi wa Russia 2022.
Forum