Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 02, 2024 Local time: 01:15

Rais wa CAR azishtumu nchi za Magharibi kuchochea uhamiaji barani Afrika


Rais wa Jamhuri ya Afrika ya kati Faustin Archange Touadera akihutubia mkutano wa 78 wa Baraza kuu la Umoja wa mataifa, Septemba 21, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Afrika ya kati Faustin Archange Touadera akihutubia mkutano wa 78 wa Baraza kuu la Umoja wa mataifa, Septemba 21, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya kati Alhamisi amezishtumu nchi za Magharibi kuchochea mzozo wa uhamiaji barani Afrika kwa kupora rasilimali za bara hilo kupitia ukoloni na utumwa.

Akiwa kwenye jukwaa la mkutano wa Baraza kuu la Umoja wa mataifa, Faustin Archange Touadera amegusia mzozo wa uhamiaji kwenye kisiwa cha Italy cha Lampedusa, ambako maelfu ya wahamiaji kutoka Afrika waliwasili wiki iliyopita.

“Vijana hawa ambao ni ishara ya leo na kesho ya bara letu wanataka sana kuingia kwenye nchi za bara la Ulaya kutafuta maisha bora,” Touadera amesema.

Ameongeza kuwa “Kuibuka kwa mzozo wa wahamiaji ni moja ya athari mbaya za uporaji wa rasilimali za nchi zilizofanywa maskini na utumwa, ukoloni na ubeberu wa nchi za Magharibi, ugaidi na mizizo ya ndani ya kivita.”

Kauli ya Touadera imetofautiana sana na matamshi ya Jumatano ya waziri mkuu wa mrengo wa kulia wa Italy Giorgia Meloni, ambaye alisema mzozo huo unasababishwa na wasafirishaji haramu wa wahamiaji na kusisitiza kwamba Afrika hakika ni bara tajiri.

Forum

XS
SM
MD
LG