Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 15:30

Rais wa C.A.R. afuta kazi baraza la mawaziri


Rais Catherine Samba-Panza wa Jamhuri ya Afrika ya Kati
Rais Catherine Samba-Panza wa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Pande zinazopigana zilitia saini makubaliano ya sitisho la mapigano Julai, lakini ghasia zikazuka upya na kusababisha vifo vya watu 22 katika mji wa Batangafo wiki jana.

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Catherine Samba–Panza amemfuta kazi waziri mkuu wake pamoja na baraza zima la mawaziri baada ya sitisho la mapigano kati ya waasi wa kiislam na wanamgambo wa Kikristo kushindikana.

Bado hajateua waziri mkuu mwingine kuchukua nafasi ya waziri mkuu aliyetimuliwa Andre Nzapayeke.

Wakati huo huo, walinda amani wa Afrika, wanasema vikosi vya Ufaransa zimeuwa waasi kadhaa wa zamani kutoka kundi la waasi wa kiislam waliowavizia katika mji wa Batangafo kaskazini mwa nchi.

Mapigano baina yao yalidumu kwa saa kadhaa.Lakini hakuna majeruhi walioripotiwa upande wa vikosi vya Ufaransa.

Jamhuri ya Afrika ya Kati imekumbwa na mgogoro wa kisiasa tangu mwaka jana, wakati waasi wa kiislam wa kundi la Seleka walimpomtimua madarakani rais na kuibua kampeni kali dhidi ya Wakristo.

Nao Wakristo walijibu kwa kuunda chama cha wanamgambo ambao wametimua karibu waislam wote kutoka mji mkuu Bangui.

Pande zote mbili zilitia saini makubaliano ya sitisho la mapigano Julai,lakini ghasia zikazuka upya na kusababisha vifo vya watu 22 katika mji wa Batangafo wiki jana.

XS
SM
MD
LG