Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 15:48

Rais wa Burundi amfuta kazi waziri mkuu


Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye Jumatano amemfuta kazi waziri wake mkuu baada ya kuonya kwamba kulikuwa na mpango wa jaribio la mapinduzi dhidi yake.

Ndayishimiye ambaye ni jenerali wa zamani katika jeshi la Burundi, amemuondoa Alain Guillaume Bunyoni.

Katika kikao cha bunge ambacho kimeitishwa kwa haraka Jumatano, wabunge wameidhinisha uteuzi wa waziri wa usalama na mambo ya ndani Gervais Ndirakobuca kuchukua nafasi ya Bunyoni, kwa kura 113 za wabunge walioshiriki katika kikao hicho, kwa mujibu wa radio ya taifa RTNB.

Habari hiyo ilithibitishwa pia na vyombo kadhaa vya habari vya mtandaoni katika taifa hilo la Afrika ya Kati.

Ndayishimiye ambaye yuko madarakani tangu mwaka 2020, hakueleza sababu za kumfuta kazi Bunyoni, lakini wiki iliyopita alisikika akionya kwamba kuna mpango wa jaribio la mapinduzi dhidi yake.

“Unadhani jenerali wa jeshi anaweza kutishiwa na wanaosema kwamba wanapanga jaribio la mapinduzi? Nani mtu huyo? Yeyote anayefikiria hilo ajitokeze, kwa nguvu za Mungu, nitamshinda, ” Ndayishimiye alionya katika mkutano wa maafisa wa serikali Ijumaa, katika mji wa kisiasa wa Gitega.

XS
SM
MD
LG