Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 13:39

Rais wa Burkina Faso achukua wadhifa wa waziri wa ulinzi


Rais wa Burkina Faso Rock Kabore kwenye picha ya awali

Rais wa Burkina Faso Roch Kabore amechukua wadhifa wa waziri wa ulinzi katika baraza la mawaziri lililobadilishwa, kwa lengo la kusitisha wimbi la mashambulizi ya wanamgambo yaliyokumba taifa hilo la Afrika magharibi, kulingana na agizo lililotangazwa Jumatano.

Makundi yanayohusishwa na al Qaeda na Islamic State na ambayo awali ngome yao ilikuwa kwenye nch jirani ya Mali, sasa yamekita mizizi kaskazini na mashariki mwa Burkina Faso wakati yakifanya mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya raia, likiwepo lile la mwezi Juni ambalo liliua zaidi ya watu 130, likisemekana kuwa ikiwa baya zaidi kwa kipindi cha miaka kadhaa.

Shinikizo liliongezeka kwa Kabore kuchukua tena udhibiti wa maeneo yanayodhibitiwa na wanamgambo hao na kumaliza mzozo wa kibinadamu, ambao umesababisha kuhama kwa zaidi ya watu millioni moja kutoka kwenye makazi yao

. Viongozi wa upinzani wamekua wakiomba serekali ijiuzulu huku wakiitisha maandamano mwishoni mwa wiki hii, dhidi ya kile wanachosema ni kushindwa kwa serekali kushughulikia mzozo huo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG