Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 16:48

Rais wa Brazil akabiliwa na mashtaka ya kumuondoa madarakani


Rais wa Brazil Dilma Rousseff akihudhuria mkutano na watalaamu wa elimu huko Planalto Palace imjini Brasilia, Brazil, April 12, 2016.
Rais wa Brazil Dilma Rousseff akihudhuria mkutano na watalaamu wa elimu huko Planalto Palace imjini Brasilia, Brazil, April 12, 2016.

Rais wa Brazil Dilma Rousseff anatarajiwa kutoa majibu yake Jumatatu kuhusu pendekezo la kufunguliwa mashtaka ya kumuondoa madarakani.

Wabunge kutoka baraza kuu la bunge walipiga kura Jumapili jioni na kuliwasilisha suala hilo kwenye baraza la Sanate ambalo litaamua iwapo Rousseff afunguliwe mashtaka.

Moja baada ya mwingine, wajumbe wote 513 walipiga kura kwa kutangaza msimamo wao kupitia kipaza sauti huku kukiwa na kelele na malumbano makali kutoka kwa wajumbe. Ilichukua saa 5 kupata theluthi mbili au kura 342 zinazohitajika kuanza shughuli ya kumshtaki Rais Rousseff ili aondolewe madarakani.

XS
SM
MD
LG