Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 27, 2023 Local time: 18:06

Rais Biden amfuta kazi mchoraji wa ramani za majengo wa bunge


Rais wa Marekani, Joe Biden, amemfuta kazi mchoraji wa ramani za majengo katika bunge, Brentt Blanton, kufuatia ripoti ya mkaguzi mkuu kuhusu masuala yanayomhusu binafsi na utendani wake wa kazi inayomtaka aondolewe.

White House imesema Jumatatu kwamba uteuzi wa Blanton umefutwa.

Hatua hiyo imetokea wakati Spika wa bunge Kevin McCathy, Jumatatu alisema kwamba hana tena imani na uwezo wa kazi wa Blanton.

Ripoti ya mkaguzi mkuu iliyotolewa mwaka jana imekuta makosa ya ukiukwaji wa kiutawala, maadili, na sera, uliofanywa na mteule huyo wa rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump.

Makosa hayo yanajumuisha pia matumizi mabaya ya magari ya serekali, na kujitambulisha vibaya kama afisa anayesimamia sheria.

Ripoti ilifichua Blanton aliruhusu mke wake na binti yake mkubwa kutumia gari lake kwa karibu maili 30,000.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG