Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 21:31

Rais wa Algeria amaliza matibabu ya Corona, afanyiwa uchunguzi zaidi


Abdelmadjid Tebboune - Rais wa Algeria

Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune amemaliza matibabu baada ya kuambukizwa virusi vya Corona, lakini ofisi yake imesema kwamba atafanyiwa uchunguzi zaidi wa kiafya.

Tebboune, mwenye umri wa miaka 75, alipelekwa ujerumani karibu wiki mbili zilizopita baada ya kugundulika kuambukizwa virusi vya Corona.

Tebboune alichaguliwa kama rais wa Algeria baada ya maandamano yaliyodumu zaidi ya mwaka mmoja yaliyomuondoa madarakani rais Abdelaziz Bouteflika.

Ameahidi kuleta mabadiliko ya uongozi na kuichumi nchini Algeria.

Mapema mwezi huu, raia wa Algeria walipitisha mabadiliko ya katiba yanayotoa mamlaka zaidi kwa bunge na waziri mkuu Pamoja na kuruhusu jeshi la nchi hiyo kushiriki katika juhudi za kuleta amani katika nchi za nje.

Tebboune ametangaza pia mipango ya kuimarisha sekta ya nshati ya Algeria na kuacha kutegemea gesi na mafuta, hatua ambayo pia inatarajiwa kubuni nafasi kadhaa za ajira katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika yenye jumla ya watu milioni 44.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG