Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 17:55

Rais Zuma akana rushwa ilitumika katika ununuzi wa silaha


Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma anasema hakukuwa na ushawishi wowote ulio na dosari katika mradi wa silaha wa serikali uliofanyika katika miaka ya 90.

Zuma ambaye alituhumiwa katika mpango huo wa silaha alitoa tangazo hilo leo alhamisi katika televisheni ya taifa. Amesema tume huru imegundua kuwa hakuna afisa yeyote aliyechukua rushwa.

Zuma alishutumiwa 2005 kwa makosa 780 ya rushwa yaliohusiana na mpango huo wa silaha. Makosa hayo yalifutwa miaka mitatu baadaye na Zuma ambaye alikuwa makamu wa Rais Thabo Mbeki akaja kuwa kiongozi wa chama cha ANC na kuchaguliwa rais 2009.

XS
SM
MD
LG