Rais wa Marekani Donald Trump amesitisha misaada kwa Ukraine, White House imetangaza Jumatatu jioni. Rais amekuwa wazi kwamba anazingatia amani, afisa wa ngazi ya juu wa utawala ameiambia VOA katika barua pepe.
Afisa huyo hakutajwa jina kama ilivyo kawaida wakati wa kuzungumza na waandishi wa habari. Anasema Tunahitaji washirika wetu waunge mkono lengo hilo pia. Tunaweka na kutathmini upya misaada yetu ili kuhakikisha kuwa inachangia suluhisho.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema katika hotuba yake ya usiku wa Jumatatu kwamba nchi yake inahitaji amani ya kweli na ya haki, pamoja na hakikisho la usalama ili kuhakikisha Russia haitoi kitisho tena kwa Ukraine katika siku zijazo.
Kulikuwa na ukosefu wa uhakika wa usalama kwa Ukraine miaka 11 iliyopita ambayo iliruhusu Russia kuanza kwa uvamizi wa Crimea na vita huko Donbas, Zelenskyy alisema. Kisha kukosekana kwa uhakika wa usalama kuliiruhusu Russia kuanzisha uvamizi kamili. Na hivi sasa kwa sababu bado hakuna uhakikisho wa usalama, Russia ndiyo inaendelea na vita hivi.
Forum