Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 05:57

Rais Trump anatishia kufungwa tena serikali kuu Marekani


Rais Trump akiwa katika mkutano wa kampeni huko Michigan. April 28, 2018

Rais wa Marekani Donald Trump anatishia kufunga serikali kuu baadae mwaka huu kama bunge la Marekani halitaidhinisha bajeti ya kutosha kwa ajili ya usalama kwenye mpaka, ikijumuisha fedha za kujenga ukuta kati ya mpaka wa Marekani na Mexico.

Mwezi uliopita, Rais Trump alitia saini mswada wa sheria wa matumizi ya dola trilioni 1.3 ambazo zinaendelea kuendesha kazi za serikali kuu hadi mwisho wa mwezi Septemba. Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni katika mji wa Washington Township, uliopo jimbo la Michigan nchini Marekani rais alisema bunge linatazamiwa kupigia kura mswaada wa sheria wa bajeti ya matumizi ya mwaka ujao hapo Septemba 28, lakini kama haitajumuisha fedha kwa ajili ya ukuta, yeye hatatia saini mswaada huo.

Ahadi ya kujenga ukuta ilikuwa ajenda kubwa wakati wa kampeni zake za urais. Hata hivyo wanachama wenzake wa Republican, huwenda wasimuunge mkono Rais Trump kama anajaribu kufunga serikali kuu kabla ya uchaguzi mdogo wa kati kati ya mwaka unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu wa 2018.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG