Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 06, 2025 Local time: 16:37

Rais Salva Kiir amfukuza kazi waziri wa mafuta Sudan Kusini


Ezekiel Lol Gatkuoth aliyekuwa mkuu wa wizara ya mafuta Sudan Kusini kwa takribani miaka mitatu
Ezekiel Lol Gatkuoth aliyekuwa mkuu wa wizara ya mafuta Sudan Kusini kwa takribani miaka mitatu

Mchambuzi wa kiuchumi mjini Juba alieleza inaonekana Ezekiel Gatkuoth alifukuzwa kazi kwa sababu hakuwa muwazi namna fedha za wizara hiyo zilivyokuwa zikitumika na huwenda amevunja sheria kuweka fedha ndani ya akaunti kwenye benki ya serikali

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir amemfuta kazi mkuu wa wizara muhimu ya mafuta ambayo inaingiza zaidi ya asilimia 90 ya mapato ya serikali ya Sudan Kusini. Kiir alichukua hatua hiyo Alhamis kumfuta kazi Ezekiel Lol Gatkuoth baada ya kuongoza wizara hiyo kwa miaka mitatu na nafasi yake kuchukuliwa na Awow Daniel Chuang.

Hata hivyo Rais Kiir hakutoa sababu za kufanya mabadiliko hayo lakini mchambuzi wa kiuchumi anayeishi mjini Juba alieleza inaonekana Gatkuoth alifukuzwa kazi kwa sababu hakuwa muwazi kuhusu namna fedha za wizara hiyo zilivyokuwa zikitumika na huwenda amevunja sheria kuhusu namna ya kuweka fedha ndani ya akaunti kwenye benki moja ya serikali.

Naye mchambuzi wa sera Augustino Ting Mayai wa taasisi ya SUDD yenye makao yake Juba alieleza kwamba katika mwaka wa kwanza wa Ezekiel Lol Gatkouth kama waziri wa mafuta, uzalishaji mafuta na mapato ni kwamba mapato ya serikali yalipunguka wakati mzozo ulipokuwa unaendelea nchi nzima pale bei ya mafuta iliposhuka kwenye soko la kimataifa.

XS
SM
MD
LG