Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 22:57

Rais Ruto akutana na Balozi wa Marekani na Seneta Chris Coons


Ruto akutana na Balozi wa Marekani Kenya na Seneta Chris Coons
please wait

No media source currently available

0:00 0:01:01 0:00

Ruto akutana na Balozi wa Marekani Kenya na Seneta Chris Coons

Siku moja baada ya kukosolewa na Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga, kuhusu maoni yake juu ya uhalali wa uchaguzi wa Kenya wa 2022, Rais William Ruto alikutana na Balozi wa Marekani Nchini Kenya Meg Whitman na Seneta wa Delaware Chris Coons huko Ikulu ya Nairobi.

Seneta Coons amekuwa nchini kuanzia wiki iliyopita kwa kile wachambuzi wanachosema ni sehemu ya juhudi za Marekani kusuluhisha mvutano kati ya Rais aliyeko madarakani Ruto na Odinga.

Viongozi hao wawili wameingia katika mvutano uliodumu miezi kadhaa kuhusiana na uchaguzi wa Agosti 2022 na hali ya uchumi ya taifa hilo.

Seneta Coons tayari alikuwa amewasiliana na Odinga, huku pande zote mbili zikiingia katika mazungumzo yanayozikutanisha pande mbili yenye lengo la kutafuta ufumbuzi juu ya kero zilizoibuliwa na upinzani.

Kufuatia mkutano wa Ikulu Ijumaa ambao ulimshirikisha Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Alfred Mutua, Rais Ruto alisisitiza nia ya dhati ya Kenya kuimarisha uhusiano na Marekani na kupanua wigo katika fursa za biashara na uwekezaji kwa raia wa nchi zote mbili.

“Ushirikiano wetu wa pamoja wenye manufaa utahusisha juhudi za kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa na kulinda mazingira,” alisema Ruto.

Kwa upande wake, Seneta Coons alieleza kuridhishwa kwake kuwa Kenya ni moja ya nchi yenye vuguvugu kubwa kabisa la demokrasia duniani.

Ikulu ya Nairobi ilisema kuwa viongozi hao wawili pia walijadili masuala ya usalama, mabadiliko ya hali ya hewa na maendeleo yaliyopatikana katika mchakato wa ugatuzi nchini Kenya.

Siku ya Alhamisi, Balozi wa Marekani nchini Kenya Whitman alikabiliwa na ukosoaji kutoka viongozi wa Azimio unaoongozwa na Raila Odinga kufuatia maoni yake kuhusu uchaguzi wa Kenya 2022 ambapo mwanadiplomasia huyo alisema ulikuwa “uchaguzi halali zaidi katika historia ya Kenya.”

Forum

XS
SM
MD
LG