Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 28, 2023 Local time: 21:50

Rais Ramaphosa atangaza janga la kitaifa kufuatia uhaba mkubwa wa umeme nchini Afrika Kusini


Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akitoa hotuba yake ya mwaka wa 2023 kuhusu hali ya taifa, Februari 9, 2023. Picha ya Reuters

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa Alhamisi alitangaza janga la kitaifa katika hatua ya kuharakisha juhudi za kukabiliana na rekodi ya uhaba wa umeme nchini humo ambao umekwamisha ukuaji wa uchumi wa taifa hilo lililoendelea zaidi kiviwanda barani Afrika.

Afrika Kusini katika miezi ya hivi karibuni ilikumbwa na moja ya mizozo mibaya ya nishati na kukatika kwa umeme kwa miaka mingi kumezidi kuwa mbaya zaidi.

Mgao wa umeme ulioratibiwa, umewekwa ili kusaidia mfumo wa umeme unaozalishwa na makaa ya mawe nchini humo uendelee kufanya kazi licha ya mahitaji makubwa.

Ramaphosa alikiri katika hotuba ya kila mwaka kuhusu hali ya taifa kwamba “ tuko katika mzozo mkubwa wa nishati.”

“Kwa hivyo tunatangaza janga la kitaifa kukabiliana na mzozo wa umeme na athari zake,” Ramaphosa alisema katika taarifa kuu ya hotuba yake ambayo ilicheleweshwa na wabunge wa upinzani ambao walijaribu kumzuia kuitoa.

Mtandao wa umeme, unaosimamiwa na kampuni ya nishati ya serikali ya Eskom, umeshindwa kuendana na mahitaji.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG