Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 20:08

Rais Ramaphosa adaiwa kutohusika na wizi wa fedha


Kundi la linalofuatilia rushwa limesema katika ripoti ya awali kwamba rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa hakuhusika katika kuficha kuhusu wizi wa kiasi kikubwa cha fedha  taslimu zilizofichwa  kwenye sofa katika nyumba yake ya kijijini.

Shutuma ya kuficha kuhusu wizi huo wa pesa hizo zilimkabili rais huyo kwa miezi kadhaa na kukaribia kumgharimu urais wake.

Vincent Magwenya, msemaji wa Ramaphosa, alisema katika taarifa yake, kwamba "tunasisitiza rais hakushiriki katika makosa yoyote, wala hakukiuka kiapo cha ofisi yake."

Ramaphosa bado atakuwa kitovu cha uchunguzi wa polisi kuhusu fedha hizo kujua zilikotokea na kile alichokifanya baada ya kuibiwa. Matokeo ya uchunguzi huo hayajatolewa hadharani, lakini baadhi ya vyombo vya habari vimepata nakala za ripoti hiyo.

Wanasema uchunguzi ulibaini kuwa mkuu wa huduma ya ulinzi wa rais hakuwajibika inavyo stahili alipoanzisha uchunguzi kuhusu wizi wa pesa hizo bila kuripoti polisi.

XS
SM
MD
LG