Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 10, 2024 Local time: 20:57

Rais Philipe Nyusi ameshinda tena uchaguzi wa urais Msumbiji


Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi na pia kiongozi wa chama tawala nchini humo cha Frelimo
Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi na pia kiongozi wa chama tawala nchini humo cha Frelimo

Rais Nyusi alisema katika muhula wake wa pili madarakani atakuwa na jukumu la kuangalia uzalishaji gesi ya asili unaoongozwa na makampuni makubwa kama vile Exxon na Total, kupambana na uasi na kutekeleza mkataba wa amani uliotiwa saini hivi karibuni

Tume ya uchaguzi nchini msumbiji-CNE imesema Rais wa Msumbiji aliyepo madarakani Philipe Nyusi ameshinda uchaguzi kwa asilimia 73 ya kura katika uchaguzi wa urais na kuchukua ushindi mkubwa huku vyama vya upinzani vinasema uchaguzi uligubikwa na wizi wa kura pamoja na ghasia.

Mgombea wa chama kikuu cha upinzani, Ossufo Momade na pia mwanachama wa zamani wa kundi la waasi la Renamo ameshikilia nafasi ya pili kwa kupata asilimia 21.88 ya kura, alisema mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini humo Abdul Carimo kwenye mkutano wa Jumapili na waandishi wa habari.

Rais Nyusi kutoka chama tawala cha Frelimo alisema katika muhula wake wa pili madarakani kwa miaka mitano atakuwa na jukumu kubwa kuangalia uzalishaji gesi ya asili unaoongozwa na makampuni makubwa ya mafuta kama vile Exxon Mobil Corp na Total, kupambana na uasi wenye itikadi kali ya ki-Islam na kutekeleza mkataba wa Amani uliotiwa saini miezi miwili iliyopita.

XS
SM
MD
LG