Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 10:59

Rais Paul Kagame aanza rasmi muhula wake wa nne


Hafla ya kuapishwa kwa Rais Paul Kagame katika uwanja wa michezo mjini Kigali, Agosti 11, 2024. Picha ya AFP
Hafla ya kuapishwa kwa Rais Paul Kagame katika uwanja wa michezo mjini Kigali, Agosti 11, 2024. Picha ya AFP

Rais wa Rwanda Paul Kagame alikula kiapo Jumapili kwa muhula wa nne, akisema amani ya kikanda ni “kipaumbele chake” katika kukabiliana na mzozo unaoendelea katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kagame alipata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa mwezi uliopita kwa kupata asilimia 99.18 ya kura, na kumpa fursa ya kukaa madarakani kwa miaka mingine mitano.

Zaidi ya marais 10 na viongozi wengine wa heshima kutoka mataifa ya Afrika walihudhuria hafla ya kuapishwa kwake katika uwanja wa michezo wenye viti 45,000 mjini Kigali, ambapo wengi walikuwa wamevalia bendera ya taifa yenye rangi ya kijani, njano na bluu.

Matokeo ya uchaguzi wa Julai 15 hayakushangaza kwa Kagame, ambaye ameliongoza taifa hilo dogo la Afrika ya kati tangu mauaji ya kimbari ya 1994.

“Amani katika kanda yetu ni kipaumbele kwa Rwanda lakini haijapatikana, hasa mashariki mwa DRC,” Kagame alisema katika hotuba yake ya kuapishwa.

“Lakini amani haiwezi kutolewa na mtu yeyote au kutoka popote hata kwa nguvu ya kiasi gani ikiwa pande husika haielewi kinachohitajika, “ alisema katika msemo ulioonekana kuilenga Kinshasa.

Rais wa Angola Joao Lourenco, ni miongoni mwa waliohudhuria hafla ya Jumapili, alitarajiwa kuwa na mazungumzo ya siri na Kagame kuhusu makubaliano ya kusitisha mapigano nchini DRC yaliyofikiwa mwezi uliopita kutokana na juhudi zake, ofisi ya rais wa Angola ilisema.

Luanda ilichangia kufikiwa kwa makubaliano hayo baada ya mkutano kati ya mawiziri wa mambo ya nje wa DRC na Rwanda.

Forum

XS
SM
MD
LG