Rais wa Sudan Omar Al Bashir amesema nchi yake haitarudi tena vitani licha ya kuongezeka kwa mvutano kati ya kaskazini na kusini wakati kura ya uhuru wa kusini ikikaribia.
Vyombo vya habari vya serikali vilimkariri Bw. Bashir akisema kwamba serikali inafanya kazi kuweka utulivu kote nchini humo.
Kusini na kaskazini wamelaumiana kwa kuweka vikosi kwenye mpaka wao kabla ya kura ya maoni itakayofanyika January 9.
Mvutano ulizidi kuongezeka Jumanne wakati waziri wa ulinzi wa Sudan akisema kwamba huenda kura ya maoni ikacheleweshwa.