Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 01:11

Rais Obama Atafuta Kura Za Vijana


Rais wa Marekani Barack Obama
Rais wa Marekani Barack Obama

Rais wa marekani Barack Obama alijaribu kuwahamasisha wapiga kura vijana katika jimbo la kati la Ohio Jumapili,wiki mbili kabla ya uchaguzi wa muhula wa kati kati wa wabunge.

Rais wa marekani Barack Obama alijaribu kuwatia nguvu wapiga kura vijana katika jimbo la kati la Ohio Jumapili,wiki mbili kabla ya uchaguzi wa muhula wa kati kati wa wabunge.

Rais Obama alikirii kuwa matatizo makubwa ya kiuchumi na kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira vinafanya uchaguzi huu kuwa mgumu kwa wanachama wa chama chake cha Democrat.

Bwana Obama aliuambia umati mkubwa wa watu katika chuo kikuu cha Ohio kwamba wapinzani wake wa chama cha Republican wanategemea wapiga kura watasahau ni nani aliyesababisha matatizo hayo pale mwanzo.

Na kwa mara ya kwanza tangu alipoingia madarakani, Rais Obama aliambatana na mkewe Michelle Obama kufanya kampeni hizo.

Uchaguzi huo wa Novemba 2 utaamua ni chama kipi kitakuwa na wingi wa viti katika baraza la Senate na lile la wawakilishi. Chama cha Republican kinalaumu sera za rais Obama kwa kutoimarika haraka kwa uchumi.

XS
SM
MD
LG