Rais wa Marekani Barack Obama amesema mashambulizi ya jeshi la Marekani huko Libya yamefanikiwa.
Katika hotuba yake ya wiki kwa taifa kupitia mtandao wa internet na radio, bwana Obama alisema ulinzi wa anga wa Libya umeondolewa .
Hotuba yake ilitolewa jumamosi ikiwa imefika wiki moja tangu Marekani na washirika wake kuanza operesheni za kijeshi kusimamia marufuku ya kutorusha ndege katika anga ya Libya, na kulinda raia dhidi ya mashambulizi ya majeshi ya Moammar Gadhafi.
Wajibu wa operesheni za Libya umehamishwa kutoka Marekani kwenda kwa washirika wake NATO.
Bwana Obama amesema hivi ndivyo jumuiya za kimataifa zinatakiwa kufanya kazi kwa mataifa mengi zaidi, na siyo Marekani pekee kuwa na wajibu na gharama za kuleta amani na usalama.
Rais wa marekani Barack Obama amesema mashambulizi ya jeshi la Marekani huko Libya yamefanikiwa.