Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 00:26

Rais Nguesso achaguliwa kwa kura zaidi ya asilimia 88


Wafuasi wa Rais Nguesso.
Wafuasi wa Rais Nguesso.

Matokeo rasmi ya uchaguzi wa rais nchini Congo Brazzaville yanaonyesha Rais aliyeko madarakani, Denis Sassou Nguesso, amechaguliwa kwa zaidi ya asilimia 88 ya kura zilizopigwa.

Hii ina maana kwamba ataendelea na utawala wake, ambao kufikia sasa, amekuwa akiongoza kwa miaka 36.

Nguesso anaongoza nchi ambayo uchumi wake umedorora kwa kipindi kirefu, licha ya kwamba inazalisha mafuta kwa wingi.

Mshindani wake wa karibu, Guy Brice Parfait Kolelas, ambaye alifariki muda mfupi baada ya vituo vya kupigia kura kufunguliwa, alipata asilimia nane tu ya kura.

Kolelas aliaga dunia kutokana na ugonjwa wa COVID-19, kwa mujibu wa taarifa ya serikali.

Wanadiplomasia na wachambuzi wa siasa, walimtarajia Ngueso, mwenye umri wa maiaka 77, kushinda kwa urahisi, hususan kwa sababu ya udhibiti alionao wa taasisi za serikali, katika taifa hilo lenye watu milioni 5.4.

XS
SM
MD
LG