Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 06:38

Rais mpya wa Angola aapishwa


FRais wa Angola Joao Lourenco
FRais wa Angola Joao Lourenco

Utawala wa muda mrefu - miaka 38 - wa  Rais wa Angola  Jose Eduardo dos Santos, ulifkia ukingoni Jumanne baada ya kuapishwa kwa Joao Lourenco kuwa rais kwenye hafla iliofanyika mjini Luanda.

Katika hotuba yake baada ya kuapishwa, Laorenco, ameahidi kupambana na rushwa na kuleta maendeleo kwa watu wa tabaka ya chini walowengi nchini humo. Harrison Kamau na maelezo zaidi

Joao Lourenco mwenye umri wa miaka 63 aliyekuwa waziri wa ulinzi wa Angola alitoa hotuba mbele ya maelfu ya watu, mjini Luanda wakati wa hafla hiyo akiapa kukabiliana na Ulaji rushwa, tatizo la umasikini pamoja na ukosefu wa ajira bila kusahau kutoa nafasi za biashara wakati akiwa rais wa wote wa Angola.

Dos Santos, ambaye hakuwa akionekana sana hadharani, amehudhuria hafla hiyo akisemekana kuwa na matatizo ya kiafya.

Kiongozi huyo wa muda mrefu alishangaza wengi baada ya kutangaza kustaafu kwake mapema mwaka huu na kusema kuwa hatashiriki kwenye uchaguzi mkuu akimchagua Lourenco kugombea nafasi yake.

Vyama vya upinzani vimesusia hafla hiyo vikidai kuwa uchaguzi ulikuwa na kasoro chungu nzima pamoja na kutokuwa na usawa wa kutumia vyombo vya habari huku kukiwa na madai ya ukandamizwaji wa wapiga kura wa mrengo wa upinzani.


UNITA, ambacho ni chama kikubwa cha upinzani, mwezi huu kimeondoa tishio lake la kutohudhuria vikao vya bunge huku mahakama ya kikatiba ikitupilia mbali madai yake ya kasoro kwenye uchaguzi.


Dos Santos ni kiongozi wa pili aliyebaki madarakani kwa muda mrefu akishindwa kwa mwezi mmoja tu na rais wa Equatorial Gunea Teodoro Obiang Nguema.

XS
SM
MD
LG