Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 10:14

Rais Lungu wa Zambia yupo nje ya nchi kwa matibabu


Rais wa Zambia, Edgar Lungu.
Rais wa Zambia, Edgar Lungu.

Rais wa Zambia, Edgar Lungu inasemakana yuko katika matibabu ya afya njeya nchi na bado anafanya kampeni kwa ajili ya kuchaguliwa tena kabla ya uchaguzi wa august 11 licha ya vyombo vya habari kuripoti kuwa hali mbaya ya kiafya imemlazimisha kwenda kwa matibabu katika nchi jirani ya Afrika kusini.

Kwa mujibu wa naibu meneja wa kampeni wa chama tawala cha Patriotic Front, bwana Frank Bwalya ripoti kuwa afya ya rais si nzuri ni njama tu za wapinzani wake kutaka kudumaza juhudi za Lungu kuchaguliwa tena.

Lungu alishiriki Alhamis katika kipindi cha televisheni kwenye kituo cha taifa cha Zambia Broadcasting Corpotation-ZBC

Tumestushwa sana kwasababu Rais Lungu amekuwa na afya nzuri, uvumi huu kuwa ni mgonjwa ni uongo mtupu. Gazeti la Post lilichapisha habari hiyo imefanya hivyo ikifahamu dhahiri kuwa azma yao siyo kuripoti ukweli ikiwa ni pamoja na afya ya rais lakini kuipotosha dunia na umma wa Zambia alisema Bwalya.

Chama kikuu cha upinzani cha United Party for National Development- UPND kimehoji tangazo la karibuni la Rais Lungu kutangaza mali zake ambayo ni moja ya matakwa makuu katika katiba kwa wagombea wote kabla ya kupitishwa kushiriki katika uchaguzi.

Lungu katika karatasi za kuwania kugombea urais alitangaza kwamba ana mali zenye thamani ya dola 4,428. Lakini UPND wanasema rais hakusema ukweli kuhusu thamani ya mali zake.

XS
SM
MD
LG