Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 21:01

Rais Kikwete azungumza na wazee wa Dar es salaam


Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania

Asema mgomo wa madaktari umezorotesha sekta ya afya nchini Tanzania

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amesema mgomo wa madaktari ulioitishwa nchini humo umezorotesha kwa kiwango kikubwa sekta ya afya na amewataka madaktari hao kutorejea tena kwenye migomo katika siku za usoni.

Akizungumza kwa mara ya kwanza jumatatu tangu kuzuka kwa migomo hiyo Rais Kikwete hata hivyo ameahidi kuyatafutia ufumbuzi matatizo yanayowakibili madaktari hao akisisitiza kwamba serikali yake imedhamiria kuboresha sekta ya afya.

Kuhusu hoja iliyotolewa na madaktari hao waliomtaka awafute kazi waziri wa afya na naibu wake , Rais Kikwete pamoja na kuelezea kutokuwepo na uwezekano wa kutokufanya hivyo kwa wakati huu lakini akasema kwamba ofisi yake inachukua kwa uzito mkubwa kuhusu hoja hiyo.

Amewataka madaktari hao kuzingatia zaidi utendaji kazi badala ya kuangalia udhaifu na tofauti binafsi za mawaziri hao.

Akizungumzia kuhusu wanaharakati ambao waliandamana mara ya kwanza madaktari walipoitisha mgomo amesema amesikitishwa na kitendo hicho kwa vile kinaonesha dhahiri kwamba hawatetea haki za binadamu kwa kuwashawishi madaktari kugoma na kusababisha vifo vya watu.

XS
SM
MD
LG