Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 16:21

Kenyatta akutana na Wajumbe wa Umoja wa Mataifa


Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amekutana siku ya Ijuma na wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini Nairobi, na kujadili azma ya serikali yake kufunga kambi ya wakimbizi ya Daadab.

Kwa mujibu wa msemaji wa Ikulu ya Nairobi, mkutano huo pia ulijadili hali ya usalama nchini Somalia kwa ujumla.

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa rais haikuelezea kama kulikuwa na makubaliano yoyote, lakini ilieleza kwamba mkutano huo ulifuatia mazungumzo ya simu kati ya rais Kenyatta na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon. Ban alitoa wito kwa Kenya kubadili uamuzi wake wa kufunga kambi hiyo ya Dadaab, ambayo ndiyo kubwa duniani, ikiwa ni hifadhi ya wakimbizi zaidi ya laki tatu na nusu.

Ujumbe huo ulijadili pia juhudi kurudisha usalama zinazofanywa na jeshi la Umoja wa Afrika huko Somalia, Amisom .

XS
SM
MD
LG