Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 19:33

Rais Kabila asema "Sitashindwa"


Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akiwasili katika gwaride mjini Kinshasa, Juni 30, 2010 (file photo)
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akiwasili katika gwaride mjini Kinshasa, Juni 30, 2010 (file photo)

Kituo cha Carter cha Marekani kinachofuatilia uchaguzi kimetoa wito wa utulivu katika siku kuelekea uchaguzi wa Novemba 28

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anasema ana hakika atashinda uchaguzi mkuu nchini humo mwezi ujao.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Kinshasa Jumanne, Rais Kabila hata hivyo aliahidi kukaa kando endapo atashidnwa, lakini alisema "Najua kitu kimoja kwa uhakika. Sitashindwa."

Mapema wiki hii, kundi linaloheshimika katika kufuatilia uchaguzi - Carter Center - nchini Marekani lilisema uchaguzi huo wa Novemba 28 unakabiliwa na vitisho vya kuwa huru na haki. Kituo hicho cha Carter kimesema tayari kimepata ripoti kadha za vitisho na umwagaji damu katika matukio ya kampeni.

Rais Kabila anakabiliwa na upinzani uliogawanyika ambao umeshindwa kuchagua mgombea mmoja kumkabili rais Kabila ambaye alichukua uongozi mara ya kwanza mwaka 2001 baada ya kuuawa kwa baba yake Laurent Kabila. Alishinda uchaguzi wa mwaka 2006.

Mmoja wa wapinzani wake wakubwa ni mkongwe wa siasa za DRC, Etienne Tshisekedi mwenye umri wa miaka 78 na ambaye alisusia uchaguzi wa mwaka 2006.

XS
SM
MD
LG