Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:53

Rais Joe Biden afuta deni la dola 10,000 kwa mamilioni ya wanafunzi wa zamani wa chuo kikuu


Rais Joe Biden akitangaza hatua yake ya kufuta deni la mkopo kwa wanafunzi wa zamani wa chuo kikuu, Agosti 24, 2022. Picha ya AP.
Rais Joe Biden akitangaza hatua yake ya kufuta deni la mkopo kwa wanafunzi wa zamani wa chuo kikuu, Agosti 24, 2022. Picha ya AP.

Rais Joe Biden Jumatano amesema serikali ya Marekani itafuta dola 10,000 katika mikopo ya wanafunzi kwa mamilioni ya wanafunzi wa zamani wa chuo kikuu wanaotaabika na madeni, akitekeleza ahadi yake aliyotoa katika kampeni ya uchaguzi wa rais ya mwaka 2020.

Hatua hiyo inaweza kuwasadia Wademocrats wenzake kupata uungwaji mkono mkubwa katika uchaguzi wa katikati ya muhula wa mwezi Novemba, lakini baadhi ya wachumi wanasema huenda hatua hiyo ikachochea ongezeko la mfumuko wa bei, na baadhi ya Warepublican katika bunge wanahoji iwapo rais ana mamlaka ya kisheria ya kufuta deni hilo.

Kufutwa kwa deni hilo kutatoa mabilioni ya dola kwa matumizi mapya ya wanunuzi ambayo yanaweza kulenga ununuzi wa nyumba na gharama nyingine za juu, kulingana na wachumi ambao wamesema hatua hiyo itaongeza kasoro mpya katika vita dhidi ya mfumuko wa bei nchini.

“Hatua hizi ni kwa ajili ya familia zinazohitaji zaidi pesa hizo , watu wa tabaka la kati na wanaofanya kazi ambao waliathiriwa vikali wakati wa janga la Covid,” Biden amesema wakati wa hotuba yake katika White House.

Aliahidi kuwa hakuna familia zenye mapato ya juu ambazo zitanufaika na hatua hiyo, akijibu ukosoaji mkubwa wa mpango wake huo.

XS
SM
MD
LG