Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 03, 2023 Local time: 20:54

Rais Joe Biden aenda Arizona kuelezea ajenda yake ya masuala ya hali ya hewa


Rais Joe Biden akiwasili kwenye Air Force One katika Uwanja wa Ndege wa Hifadhi ya Kitaifa ya Grand Canyon, Jumatatu, Agosti 7, 2023.AP

Biden ambaye anawania muhula wa pili anapanga kutumia safari hiyo kuangazia jinsi utawala wake umefanya uwekezaji wa kihistoria katika hali ya hewa uhifadhi na nishati safi kwa mujibu  wa White House.

Rais Joe Biden alisafiri kwa ndege hadi Arizona Jumatatu, kuelezea ajenda yake ya hali ya hewa katika akitembelea majimbo mbali mbali ambayo yanapitia kipindi kibaya cha wimbi la joto la kali lililoweka rekodi.

Kituo chake cha kwanza katika ziara yake kitakuwa Grand Canyon ambako kwa mujibu wa vyombo vya habari kadhaa vya Marekani huenda akataja mnara mpya wa kitaifa.

Tamko hilo litazuia mara moja uchimbaji wa uranium katika eneo hilo marufuku iliyotafutwa kwa miongo kadhaa na makabila ya wenyeji ya Marekani.

Biden ambaye anawania muhula wa pili anapanga kutumia safari hiyo kuangazia jinsi utawala wake umefanya uwekezaji wa kihistoria katika hali ya hewa uhifadhi na nishati safi, kwa mujibu wa White House.

Pia atakuwa huko Arizona siku ya Jumanne kabla ya kusafiri siku inayofuata katika jimbo jirani la New Mexico.

Forum

XS
SM
MD
LG