Takriban wagombea 20 kutoka vyama 26 vya kisiasa wamejitokeza kutaka kuchukua nafasi ya Sirleaf katika uchaguzi wa mwezi ujao, ikiwa ni pamoja na wanasiasa maarufu.
Hata hivyo, baadhi ya wapiga kura bado hawajaamua ni nani wanayemtaka kuchukua nafasi hiyo.
Ingawa Sirleaf amepata sifa kimataifa kwa kuimarisha nchi hiyo iliyokumbwa na vita, utawala wake unakabiliwa na tuhuma za ulaji rushwa.
Mmoja wa wagombea wanaoongoza ni aliyekuwa afisa mkuu wa kampuni ya Cocacola, Alexander Cummings.
Waliberia watapiga kura tarehe 10 mwezi ujao. Sirleaf ameongoza nchi hiyo tangu mwaka wa 2005.
Facebook Forum