Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:43

Rais Buhari wa Nigeria alaani mauaji ya waumini kwenye kanisa la kikatoliki Kusini Magharibi mwa nchi


Rais Muhammadu Buhari akihudhuria mkutano wa viongozi wa ECOWAS mjini Accra Ghana
Rais Muhammadu Buhari akihudhuria mkutano wa viongozi wa ECOWAS mjini Accra Ghana

Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria amelaani kile alichokielezea ni "muaaji ya kikatili ya waumini," wakati watu waliokuwa na bunduki walipowashambulia waumini kwa risasi katika kanisa moja mjini Owo, katika jimbo la Ondo.

Washambuliaji wasiojulikana waliingia kwenye kanisa la Kikatoliki la Saint Francis na kuwashambulia kwa bunduki na vipulizi waumini waliokua wanahudhuria ibada ya asubuhi Jumapili.

Adelegbe Timileyin mbunge wa wilaya ya Owo katika bunge la Nigeria, amewaambia waandishi habari kwamba kasisi aliyekuwa anaongoza ibada ametekwa nyara na miongoni mwa waliofariki walikuwemo watoto wengi.

Maafisa wa usalama hawajatoa idadi ya waliofariki, lakini Timileyin anasema anadhani hadi watu 50 wameuliwa, ingawa anasema kwamba huenda idadi itakuwa kubwa zaidi.

Papa Francis aliyearifiwa kuhusu shambulio hilo alitoa taarifa akisema "ninawaombea waathirika na nchi nzima, kutokana na msiba huu uliotokea wakati wa kusherehekea Pentekoste."

Haijafahamika bado nani aliyehusika na shambulio hilo ambalo ni nadra kutokea kwenye jimbo hilo, licha ya kwamba baadhi ya majimbo ya Nigeria yamekua yakishuhudia mashambulio ya mara kwa mara yakifanywa na wanamgambo wenye itikadi kali na magenge ya wahuni.

XS
SM
MD
LG