Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 16:39

Rais Biden kukutana na Rais Ramaphosa wa Afrika Kusini, White House


Picha ya Maktaba: Rais wa Marekani, Joe Biden, akiwa na rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa wakati wa mkutano wa G7 uliofanyika Cornwall, England, Juni 12, 2021. Picha na Leon Neal (Pool via AP)
Picha ya Maktaba: Rais wa Marekani, Joe Biden, akiwa na rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa wakati wa mkutano wa G7 uliofanyika Cornwall, England, Juni 12, 2021. Picha na Leon Neal (Pool via AP)

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, atakutana na rais wa Marekani, Joe Biden, White House, siku ya Ijumaa ambapo masuala ya biashara, nishati na usalama yakiwa ni agenda kuu.

Kile ambacho hakipo katika program rasmi, lakini kuna uwezekano wa kujadiliwa wachambuzi wanasema ni kuhusu masuala ya kidemokrasia na tofauti juu ya uvamizi wa Russia nchini Ukraine.

Ziara ya kwanza ya Ramaphosa kwenda White House inafanyika wakati utawala wa rais Biden, unatafuta namna ya kushirikiana tena na Afrika ikichochewa na ziara ya karibuni ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, barani Afrika ambapo alizindua mkakati mpya wa Washington kwa Afrika.

Wakati wa ziara yake ya Agosti, waziri Blinken alisisitizia kwamba Marekani inaichukulia Afrika kama mshirika mwenye hadhi sawa.

Hata hivyo, katika mkutano wao wa Pretoria, waziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusini, Naledi Pandor, aliyashutumu mataifa ya magharibi kwa kuionea Afrika katika kuyataka mataifa yake kukemea uvamizi uliofanyika Ukraine.

Bob Wekesa ni mkurugenzi wa kituo cha Afrika kwa masomo ya Marekani katika chuo kikuu cha Witwatersrand, anasema.

“Katika mkutano ilikuwa wazi kabisa kwamba Afrika Kusini na Marekani zilikuwa katika njia mbili tofauti kuhusiana na masuala mengi.”

Anasema kuna uwezekano Ukraine ikajitokeza tena wakati wa rais Biden na Ramaphosa watakapo kutana Ijumaa, na ubashiri ni kwamba viongozi hao wawili watakuwa na mjadala mgumu wa masuala mbali mbali.

“Marekani kuchukuwa msimamo wa wazi kuiunga mkono Ukraine na kama kutaka kuwaondoa wanajeshi wa Russia, Ukraine, itakuwa inajaribu kuishawishi Afrika Kusini ingawa itakua vigumu kubadilisha msimamo.”

Afrika Kusini haikushiriki kupiga kura Umoja wa Mataifa mapema mwaka huu kushutumu uvamizi wa Russia.

Baadaye rais Biden, alimpigia simu rais Ramaphosa. Taarifa ya baadaye ya White House baada ya simu hiyo ilieleza rais Biden alisisitiza umuhimu wa kuwa wazi, na mwitikio wa pamoja wa kimataifa dhidi ya uchokozi wa Russia kwa Ukraine.

Steven Gruzd, mkuu wa programu ya utawala wa Afrika na diplomasia katika taasisi ya masuala ya kimataifa, amesema rais Ramaphosa na rais Biden watajadili masuala mengine, lakini nyongeza ya Ukraine haiwezi kuepukika. Anasema

“Katika agenda itakuwa biashara na uwekezaji, masuala kama mabadiliko ya hali ya hewa, hali ya chakula, amani na usalama katika Afrika yatajadiliwa, lakini yale yasiyo rasmi itakuwa ni vita vya Ukraine na mitazamo tofauti kati Afrika Kusini na Russia na hasa mgogoro wenyewe.”

Gruzd mesema anatarajia muswada ya kukabiliana na shughuli za Russia, barani Afrika, ambao umepitishwa na baraza la wawakilishi la Marekani na sasa ukisubiri kupitishwa na baraza la Seneti, utajitokeza katika mazungumzo ya viongozi hao wawili.

Mataifa ya Afrika yanaona muswada huo utaweka vikwazo kwa mataifa yanayofanya biashara na Russia ikiwa ni jaribio la kuyaadhibu kwa kutopiga kura pamoja na Marekani kuhusiana na suala la Ukraine.

Mwei Desemba, rais Biden anatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano na viongozi wa Afrika hapa Washington.

XS
SM
MD
LG