Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:23

Rais Biden atangaza mpango wa kukabili mabadiliko ya hali ya hewa


Rais Joe Biden akihutubia mkutano wa viongozi wa nchi za Amerika huko Los Angeles.
Rais Joe Biden akihutubia mkutano wa viongozi wa nchi za Amerika huko Los Angeles.

Rais Joe Biden ameelezea mpango wake wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuimarisha nishati mbadala katika mabara ya Amerika, alipokuwa ana hutubia mkutano wa viongozi wa nchi za Amerika huko Los Angeles. 

Akizungumza kwenye kikao cha Alhamisi, Rais Biden amesema mpango huo utabuni nafasi nzuri za ajira katika nchi za Amerika Kusini na Kati. Lakini wachambuzi wanasema anakabiliwa na vizingiti vingi kati ya mawazo na utekelezaji.

Uharibifu wa misitu na mioto ya misitu inachangia katika changamoto za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa zinazokumba mataifa ya Amerika Kusini na Caribbean. Lakini Rais Biden amesema kurekebisha madhara yanayotokana na mabadiliko hayo ni nafasi nzuri alipokuwa anapendekeza kwenye mkutano wa viongozi wa nchi za mabara ya Amerika, mipango ya kupunguza hali ya kutegemea mafuta ghafi.

Joe Biden, Rais wa Marekani, “Ninaposikia hali ya hewa, nina fikiria ajira, mishahara mizuri, kazi za viwango vya juu ambazo zitasaidia kuharakisha mpito kuelekea uchumi wa kijani wa baadae na kuzalisha ukuwaji endelevu.”

Kwenye mkutano huo wa viongozi mjini Los Angeles, Biden aliwakaribisha wakuu wa mataifa 23 kujadili ukuaji wa uchumi endelevu, uhamiaji, afya na changamoto nyingine katika kanda yao.

Mpango wake wa mabadiliko ya hali ya hewa una lengo la kuhamasisha uwekezaji katika nishati safi. Wachambuzi wanasema njia ni ndefu kati ya mawazo hayo na matokeo yake.

Luiza Duarte, msomi kwenye kituo cha Wilson, “Nina dhani mikutano hiyo ya viongozi kama tunavyofahamu, inahusu matangazo chungu nzima, na si daima matangazo hayo yanaleta sera thabiti na maendeleo thabiti kwa kanda zima.”

Mipango hiyo inaweza kukabiliwa na upinzani kutoka kwa rais Jair Bolsonar wa Brazil, kiongozi anatilia shaka dhana ya mabadiliko ya hali ya hewa, ambaye anaripotiwa kuomba mkutano wa ana kwa ana na Rais Biden kama sharti kabla ya kuhudhuria mkutano wa viongozi.

Jair Bolsonaro, Rais wa Brazil, “Tunafana kila tuwezalo, ili tukidhi mahitaji yetu, tuimarishe maslahi yetu. Na vile vile kukidhi mahitaji ya dunia kwa ujumla. Kama nilivyosema awali, sisi ni mfano katika macho ya dunia inapohusiana na ajenda ya kulinda mazingira”.

Kwa ujumla nchi za kanda hii zinafahamu haja ya kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa, hasa mataifa ya visiwa vya Caribbean yanayokabiliwa na hatari ya moja kwa moja ya kuongezeka viwango vya bahari ansema profesa Enrique Dussel Peters wa chuo kikuu cha Mexico.

Enrique Dussel Peters, profesa wa chuo kikuu cha Mexico, “Ni dhahir kwamba hata mataifa maskini yanabidi kuwekeza kutokana na rasilmali zao wnyewe. Ikiwa Marekani itatoa msaada , basi ni jambo zuri kabisa.”

Ijumaa viongozi kwenye mkutano huo watazingatia suala la uhamiaji.

XS
SM
MD
LG