Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 01, 2022 Local time: 18:59

Rais Biden atangaza hatua za utendaji zinazolenga kuondoa uharamu wa matumizi ya bangi Marekani


Mwandamanaji anapeperusha bendera yenye majani ya bangi iliyoonyeshwa juu wakati wa maandamano ya kutaka kuhalalishwa kwa bangi, nje ya Ikulu ya Marekani Aprili 2, 2016, mjini Washington. Rais Joe Biden anawasamehe maelfu ya Wamarekani waliopatikana na hatia ya wa bangi.

Rais Joe Biden siku ya Alhamisi alitangaza hatua mpya za utendaji zinazolenga kuondoa uharamu wa matumizi ya bangi Marekani , ambayo sasa ni halali kwa matumizi ya matibabu katika majimbo 37 na inapatikana kwa matumizi ya burudani katika majimbo 19, ikiwa ni pamoja na makao makuu na Guam.

Katika ujumbe wa video uliorekodiwa, Biden alisema alikuwa akitangaza, kupitia amri ya kiutendaji, msamaha kwa makosa yote ya awali ya serikali kuu ya kumiliki bangi hiyo.

Msamaha huo unaweza kuwasaidia zaidi ya Wamarekani 6,500, maafisa wa White House waliwaambia waandishi wa habari. Lakini waliongeza kuwa hukumu nyingi za bangi hutokea katika ngazi ya serikali za majimbo na kupelekea angazo la pili la Biden, ambalo linatoa wito kwa magavana kutoa msamaha kwa makosa ya kumiliki bangi katika majimbo yao.

Biden pia siku ya Alhamisi alielekeza mapitio ya serikali kuu ya jinsi bangi imepangwa kutumika chini ya sheria ya serikali kuu. Kwa sasa imeainishwa na Utawala wa Usimamizi wa madawa kama dawa ya daraja la kwanza, inayofafanuliwa kama dawa zisizo na matumizi ya matibabu na uwezekano mkubwa wa matumizi mabaya, na kuiweka katika kiwango sawa na heroin na LSD.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG