Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 27, 2022 Local time: 04:06

Rais Biden asaini amri ya kiutendaji itakayowajibisha polisi wanaowatesa raia


Rais Joe Biden akisaini kwenye White House, amri ya kiutendaji ambayo itawajibisha polisi wanaofanya makosa ya kuwatesa raia. May 25, 2022, picha ya AP.

Rais wa Marekani Joe Biden Jumatano amesaini amri ya kiutendaji ambayo anasema italeta uwajibikaji zaidi na ufanisi kwa polisi, katika kumbukumbuku ya mwaka wa pili ya mauaji ya Georges Floyd, Mmarekani mweusi mkazi wa mji wa Minneapolis, aliyeuawa na afisa wa polisi mzungu.

“Ni mfano wa kile tunachoweza kufanya pamoja kuiponya nafsi ya taifa hili,” Biden amesema.

“Ili kukabiliana na hofu kubwa na kiwewe, uchovu ambao Wamarekani weusi wamepitia kwa vizazi, na msururu wa maumivu ya kibinafsi na hasira ya umma, ni ishara chanya ya maendeleo katika miaka ijayo.”

Amri hiyo ya kiutendaji inaunda hifadhi ya kitaifa ya takwimu inayoorodhesha makosa ya polisi, inaagiza uchunguzi wa kina wa haraka, inaagiza polisi kuwa kila mara na kamera zinazowarekodi wakiwa katika shughuli zao, na inapiga marufuku polisi kutumia nguvu za kupindukia, kati ya mambo mengine.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG