Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 12:21

Rais Biden anasema utawala wake utasambaza chanjo milioni 80 kote duniani


Rais wa Marekani, Joe Biden anasema Marekani itasambaza chanjo za COVID duniani kote
Rais wa Marekani, Joe Biden anasema Marekani itasambaza chanjo za COVID duniani kote

Hivi sasa utawala wa Biden unapeleka chanjo za COVID-19 nchini Taiwan. Tangazo linakuja wakati takribani asilimia 45 ya wamarekani wamepatiwa chanjo kamili dhidi ya virusi vya Corona kulingana na kitengo kinachofuatilia virusi vya Corona kutoka chuo kikuu cha John Hopkins cha Marekani

Marekani inasema inapeleka chanjo milioni 2.5 za COVID-19 kwenda Taiwan, ikiongeza kwa kiasi kikubwa ahadi yake ya awali ya kutuma dozi 750,000.

Rais wa Taiwan, Tsai Ing-wen alisema kuongezeka kwa idadi ya dozi, ni ishara ya urafiki unaosonga mbele. Rais wa Marekani Joe Biden anasema utawala wake utasambaza chanjo milioni 80 kote duniani.

Dozi hizo ni sehemu ya msaada wa dozi milioni 500 ambazo Marekani imejitolea kuchangia kwa takribani maeneo 100 kwa zaidi ya miaka miwili ijayo.

Utawala wa Biden unapanga kuchangia dozi milioni 200 mwaka huu na dozi nyingine milioni 300 katika mwaka 2022 kwenda nchi 92 pamoja na Umoja wa Afrika.

Data za watu waliopata angalau dozi moja ya chanjo ya COVID-19 , Jun 9, 2021
Data za watu waliopata angalau dozi moja ya chanjo ya COVID-19 , Jun 9, 2021

Tangazo linakuja wakati takribani asilimia 45 ya wamarekani wamepatiwa chanjo kamili dhidi ya virusi vya Corona kulingana na kitengo kinachofuatilia virusi vya Corona kutoka chuo kikuu cha John Hopkins cha Marekani.

Kwa upande mwingine India yenye idadi ya watu zaidi ya bilioni 1.3, imetoa chanjo zaidi ya asilimia tatu kwa watu wake.

Wizara ya afya nchini India ilisema Jumapili kwamba ilikuwa imerekodi zaidi ya kesi mpya 58,000 katika kipindi cha saa 24 zilizopita. India imerekodi karibu kesi milioni 30 za virusi vya Corona.

Wakati huo huo, Marekani pekee ina zaidi ya kesi milioni 33.5. Virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19.

XS
SM
MD
LG