Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 20, 2024 Local time: 15:21

Rais Biden akutana na waziri mkuu wa Uholanzi


Rais wa Marekani, Joe Biden na waziri mkuu wa Uholanzi, Mark Rutte, walipo kutana White House.
Rais wa Marekani, Joe Biden na waziri mkuu wa Uholanzi, Mark Rutte, walipo kutana White House.

Katika mkutano wake wa Jumanne na waziri mkuu wa Uholanzi, Mark Rutte, wa White House, rais wa Marekani, Joe Biden, alionekana kutofanikiwa kuishawishi Uholanzi kuunga mkono masharti mapya ya Marekani, kwa China, ikiwa ni sehemu muhimu ya mkakati wa Washington wa upinzani na Beijing.

Wakati wa mkutano wa muda mfupi mbele ya wanahabari kabla ya mkutano wao, rais Baiden alisema yeye na waziri mkuu Rutte wamekuwa wakifanyakazi pamoja ya kuweka uwazi na uhuru katika eneo la Indo-Pacific, kukabiliana na changamoto za China.

Msemaji wa White House, Karine Jean-Pierre, Jumanne, amesema utawala wa rais Biden utaendelea na juhudi zake.

Amesema kwamba hawalazimishi washirika wao ama wadau, bali wanajadiliana nao kwa ukaribu na kuacha wafanye maamuzi yao wenyewe.

XS
SM
MD
LG