Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 03:24

Rais Biden aahidi kuwa utawala wake utajenga upya Puerto Rico


Rais wa Marekani Joe Biden, akiwa na Mke wake Jill Biden, akitoa hotuba kuhusu Kimbunga Fiona, Jumatatu, Oktoba 3, 2022, huko Ponce, Puerto Rico.(AP Foto/Evan Vucci)
Rais wa Marekani Joe Biden, akiwa na Mke wake Jill Biden, akitoa hotuba kuhusu Kimbunga Fiona, Jumatatu, Oktoba 3, 2022, huko Ponce, Puerto Rico.(AP Foto/Evan Vucci)

Rais wa Marekani Joe Biden alitembelea eneo la lililoharibiwa na kimbunga Fiona Jumatatu huko Puerto Rico na kuahidi msaada wa zaidi ya dola milioni 60 kusaidia eneo hilo ambalo ni himaya ya  Marekani,  baada ya dhoruba ya mwezi uliopita.

"Tunawekeza katika barabara za Puerto Rico, madaraja, usafiri wa umma, bandari, viwanja vya ndege, usalama wa maji na mtandao wa kasi," Biden alisema katika mji wa kusini wa Ponce, ulioathiriwa sana na kimbunga

Aliahidi kuwa utawala wake umejitolea kujenga upya Puerto Rico na akasema atahakikisha inapata "kila dola moja iliyoahidiwa" baada ya dhoruba.

"Hatuondoki hapa maadamu mimi ni rais, hadi kila jambo tunaloweza kufanya lifanyike," Biden alisema.

White House ilisema kwamba ufadhili mpya wa dola milioni 60 utatoka kwenye sheria ya miundombinu iliyopitishwa na wabunge wa pande zote mbili mwaka jana na itatumika kuimarisha barabara na kuta za kuzuia mafuriko na pia kuunda mfumo wa kutoa maonyo ya mafuriko katika eneo hilo.

Kimbunga Fiona kilipiga Puerto Rico Septemba 18 mwaka huu na kukata umeme katika kisiwa kizima

XS
SM
MD
LG