Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 14, 2024 Local time: 17:20

Rais Magufuli aonya uhuru wa vyombo vya habari unakikomo


Rais John Magufuli
Rais John Magufuli

Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amewaonya wamiliki wa vyombo vya habari Ijumaa akisisitiza kuwa uhuru wao unakikomo.

“Nawaambia wamiliki wa vyombo vya habari, “be careful,” (chukueni tahadhari), “watch it” (angalieni) kama mnafikiri mna freedom ya namna hiyo “not to that extent” (sio kwa kiwango hicho).”

Rais John Magufuli amesema hayo baada ya kuwaapisha watu kadhaa na miongoni mwao ni Waziri ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harisson Mwakyembe baada ya kuondoshwa Nape Nnauye katika nafasi hiyo.

Rais pia alimwapisha Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamaganda Kabudi akiiziba nafasi ilioachwa na Dkt Mwakyembe.

Pia katika tafrija hiyo fupi Katibu Mkuu wa Ikulu na mabalozi mbalimbali wanaowakilisha Tanzania walikuwa katika wale walioapishwa.

Rais Magufuli baada ya kuwapongeza wote walioteuliwa amewaambia wasitegemee mazuri sana kwani kazi huwa zina lawama hasa kwa Tanzania ambapo kuna kundi la watu ambao siku zote kazi yao ni kulalamika.

Amedai Mwakyembe kwa mujibu wa mitandao ya jamii iliripoti asingekuja kuapishwa na kuwa wapo walioposti kuwa Kinana angeongea leo kwenye vyombo vya habari na kinyume cha hilo kwani alikuwa amemtuma India kwa matibabu.

Rais Magufuli amemwamrisha Waziri wa Habari Dkt Harrison Mwakyembe kuvichukulia hatua za kisheria vyombo vyote venye nia ya uchochezi.

"Kila kitu chenye nia ya uchochezi fulani fulani, wao ndio stori. Sasa Mwakyembe kafanye kazi. Nataka ukafanye kazi. Kama wapo waliokuwepo waliokuwa wanashindwa kuchukua hatua wewe kachukue," amesema Dkt Magufuli alipokuwa anamwapisha Dkt Mwakyembe kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Rais amesema kuwa: “Nchi yetu huko nje ina sifa kubwa sana, juzi tu hapa amekuja rais wa Benki ya Dunia na amekubali kutupatia Shilingi Trilioni 1.74 na pia Benki ya Dunia.”

Ameongeza kuwa “Benki ya Dunia ipo katika mchakato wa kutupatia fedha zingine Shilingi Trilioni 2.8 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.”

XS
SM
MD
LG