Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 18:38

Rais Alpha Conde ashinda uchaguzi Guinea - Tume


Rais wa Guinea Alpha Conde.
Rais wa Guinea Alpha Conde.

Tume ya uchaguzi nchini Guinea-Conakry ilitangaza Jumamosi kwamba Rais Alpha Conde alishinda uchaguzi wa tarehe 18 mwezi huu, kwa kupata asili mia 59.5 ya kura zote zilizopigwa, kwa mujibu wa matokeo yote ya awali.

Ushindi huo, ambao ni lazima uidhinishwe na mahakama ya katiba, unampatia rais huyo mkongwe, mwenye umri wa miaka 82, muhula mwingine uongozini, kufuatia uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali, huku upinzani ukipinga kushiriki kwa rais huyo kwenye kinyang’anyiro hicho.

Hata hivyo, Mpinzani mkuu wa Conde, Cellou Dalien Diallo, amesema ana ushahidi wa udanganyifu katika mchakato huo wa uchaguzi na kwamba atawasilisha hoja ya kupinga matokeo hayo mahakamani.

Tume hiyo ilisema Diallo alipata asili mia 33.5 ya kura. Matokeo ya uchaguzi huo yamekuwa yakitolewa kwa awamu, lakini kwa kiasi kikubwa, yamekuwa yakionyesha kwamba Rais conde alikuwa akielekea kushinda, hali ambayo imepelekea maandamano katika ngome za upinzani, ambako takriban watu 17 wamepoteza maisha yao.

Kwa mujibu wa katiba, Diallo ana siku nane kuwasilisha malalamishi mahakamani baada ya tume kutangaza matokeo hayo.

XS
SM
MD
LG